Vifuatavyo ni vegozo unavwoweza kutumia kuelezea muundo wa shairi.
Je, shairi lina beti ngapi?
→ Hesabu idadi ya beti (mistari ya mashairi inayounda kipande kamili).
Kila ubeti una mishororo mingapi?
→ Angalia idadi ya mistari (mishororo) katika kila ubeti.
Kila mshororo una vipande vingapi?
→ Tambua kama kila mshororo una sehemu moja, mbili, au zaidi (vipande).
Je, mshororo wa mwisho unarudiwa au ni kitu?
→ Angalia ikiwa mshororo wa mwisho unajirudia katika kila ubeti au ni kituo.
Mshororo wa mwisho umefupishwa?
→ Hakiki kama mshororo wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo mingine katika ubeti.
Mishororo ina vina vingapi?
→ Hesabu idadi ya vina vya ndani na vya nje kwa kila mshororo.
Mpangilio wa vina vya kati na nje ni upi?
→ Eleza jinsi vina ndani na nje vimepangika
Kuna neno/kifungu cha maneno kimerudiwa katika beti zote?
→ Chunguza kama kuna maneno au vifungu vinavyorudiwa kwa beti zote.